Welcome, 2zone & company-We are registered computer resellers, software developer, computer technicians, Advertisements & event orgernizers and all ICT consultations.

.........We are here to serve.

Sunday, 8. April 2012 - 17:55 Uhr

Ifahamu Amazon Kindle

Tangu Kuingizwa sokoni mwaka 2007, Kindle imajizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya  majarida, vitabu, blogs na usomaji wa habari mbalimbali kutoka vyombo vya habari vianavyotoa habari katika mitandao.

 

Kwa ufupi KINDLE ni kifaa, tofauti kidogo na iphones au smartphones nyingi kutokana na uwezo wake wa kutoa muonekano halisi wa karatasi kielectroniki na wakati huo huo kutumia umeme kidogo kuliko smartphones.

 

Kuanza kwa matumizi ya kifaa hiki kumeleta mabadiliko makubwa kihistoria, kwa mfano katika miezi mitatu mfululuzo mwaka 2010, mauzo ya vitabu halisi katika mtandao yalipitwa kwa kiasi kikubwa na mauzo ya ebooks na pia uwezo wake wa kuhifadhi au kukaa na chaji hadi kufikia mwezi mmoja(kindle ya kizazi cha nne)

 

Kwa sasa Kindle iko katika kizazi cha nne, (fourth generation) mabadiliko yaliyotokana na kuongezeka kwa vitu mbalimbali kutoka kizazi kimoja hadi kingine, tofauti kubwa zikiwa katika ufanisi, kizazi cha kwanza hadi cha nne Kindle zimebadilika kwa kuongeza ufanisi muhimu ikiwa ni ukubwa wa umbile, labda na mbwembwe pale unapogeuza Kindle kutoka portrait kwenda landscape na kurasa unayo soma hufanya vivyo hivyo, uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu na kuchakata data, kuwekwa kwa baobonye rahisi (Keys), na screen touch. Mabadiliko haya ndiyo pia yanayo saidia kuzipa majina, mfano, Kindle ya kizazi cha nne inaitwa Kindle touch, kuonyesha uwezo wake wa screen touch.

 

Naam ni wakati wa wasomi na wanafunzi, hususani tunaojari mazingira Kupunguza matumizi ya Karatasi na kutumia vitabu vya kielectroniki, yaani ebooks kama sijakosea, Kutokana na ufanisi wa vifaa hivi,

Kufahamu umuhimu wa kifaa hiki labda turejee takwimu za mauzo ambapo baadhi ya vyanzo vinavyosadidkika kutoka ndani ya AMAZON, wamiliki, watengenezaji(chini ya Lab126) na wauzaji wa teknolojia hii, mpaka kufikia 2009 takribani Kindle milioni tatu zilikwisha nunuliwa, japo mwaka mmoja tuu tangu kuanza kuuzwa rasmi.

Tuma Order yako kwa sales.2zone@gmail.com Ujipatie Kindle yako mapema, pia kupata bei na aina zilizopo.

 

 

 


Tags: third generation kindle touch kindle dx kindle amazon kindle 

1593 Views

Publish commentSend comment...